Wananchi washinda Juani Siku Nzima kujua Hatma Ya mtendaji huyo
Wananchi wa Kijiji cha Itambo Mkoani Njombe walalamikia utendaji kazi wa
Afisa Mtendaji wa Kijiji hicho. Kaimu Afisa Tarafa ya Mdandu Bwana Benson Wandelage wa Mwanzo Kulia akiandika Malalamiko ya Wananchi wa Kijiji cha Itambo Wilaya ya Wanging'ombe.
Hapa wakiwa kwenye Mkutano ulioitishwa na Afisa Tarafa kwa Niaba ya DC Wa Wilaya ya Wanging'ombe.
Na Prosper Mfugale.
Wakizungumza Wakati wa Ziara ya Kaimu Afisa Tarafa ya Mdandu,Wananchi Hao Wamesema Kumekuwa na Hali ya Mkanganyiko wa Taarifa za Fedha Wanazochangia na Kuongeza Kuwa Viongozi wa Kijiji Wamekuwa Wakiongoza Kijiji Hicho Kwa Mabavu.
Wamesema Kumekuwa na Tatizo la Kutosomwa Kwa Taarifa za Mapato na Matumizi Kwa Muda Mrefu Pamoja na Kumtaka Kaimu Afisa Tarafa Kumuondoa Afisa Mtendaji wa Kijiji Hicho Ikiwa ni Kwa Kile Walichokiita Kuwa ni Kushindwa Kuongoza Kijiji Hicho na Kushindwa Kusimamia Shughuli za Kimaendeleo
Kwa Upande wake Kaimu Afisa Tarafa ya Mdandu Bwana Benson Wandelage Ameuagiza Uongozi wa Kijiji Hicho Kutafutia Ufumbuzi Kero na Malalamiko ya Wananchi Pamoja na Kuwasomea Taarifa za Mapato na Matumizi Jumapili Ijayo
Hata hivyo Licha ya kuwepo kwa Taarifa ya ziara ya Afisa Huyo kufika Kijijini hapo Lakini Afisa Mtendaji wa Kijiji hicho hakuweza kuhudhuria Mkutano huo kwa Madai ya kuwa Nje ya Kijiji kikazi.