Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Article 1

$
0
0



Gari la Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji Kilifanikiwa Kufika Japo kwa Kuchelewa na Kisha Kuzima Moto Huo kwa Kushirikiana na Wananchi.

Na Gabriel Kilamlya NJOMBE,

Wananchi wa Mtaa wa Mjimwema na Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji Mjini Njombe Wamefanikiwa Kuzima Moto Uliokuwa Unawaka na Kuuguza Zaidi ya Hekari 20 za Mashamaba ya Miti Yaliyokaribu na Mto Eneo la Mjimwema.

Wakieleza Chanzo cha Moto Huo Baadhi ya Mashuhuda Wamesema Umetokana na Mtoto Tony Mligo  Mwanafunzi wa Darasa la Pili Katika Shule ya Msingi Mjimwema Mjini Wakati Akiwa  Kwenye Shughuli za Kuandaa Shamba Ambaye Alikimbia Baada ya Kutokea Moto.

Kwa Mujibu wa Dina Mligo Ambaye ni Mdogo wa Tony Amesema Kaka Yake Tony Mligo Alikuwa Akizuiliwa Kuwasha Moto  Lakini Hakuta Kusikia Hali Iliyopelekea Moto Huo

Kuzuka na Kuunguza Miti ya Mbalimbali Ambayo Thamani Yake Haijafahamika.

Kwa Upande Wake Mwenyekiti wa Mtaa wa Mjimwema Andreas Mligo Amesema Licha ya Serikali ya Mtaa Kutoa Elimu na Kuzuia Shughuli za Uandaaji wa Mashamba Kwa Kuchoma Moto Bado Baadhi ya Wananch Wanakaidi Agizo Hilo.

Miongoni Mwa Wananchi Walioathirika na Moto Huo ni Bwana Fortunatus Mbilo Ambaye Ameuliwa Shamba la Miti la Hekari Sita.

Hivi Karibuni Serikali Wilayani Njombe Amepiga Marufuku Kuanda Mashamba Kwa Kuchoma Moto Pamoja na Kuendesha Shughuli za Kilimo Karibu na Vyanzo Vya Maji Lakini Bado Baadhi ya Wananchi Wanoaoneka  Kukaidi Agizo Hilo.

............................................................................................

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Trending Articles