Na Gabriel Kilamlya Njombe
Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Imejihakikishia Kupata Shilingi Milioni 344.4 Kwa Mwaka Kutoka kwenye Vyanzo vya Mapato Mbalimbali Kutoka Kwenye Kata Tatu zilizobinafsishwa Vyanzo Vyake.
Kata Hizo ni Zile za Matembwe,Kidegembye na Ikuna Ambazo Kuanzia Septemba Mosi Mwaka Huu Vyanzo vyake vya Mapato Vyote Vimebinafsishwa Ili Kuongeza Kiwango cha Ukusanyaji Mapato Pamoja na Kuwapunguzia Majukumu ya Kusimamia Shughuli za Maendeleo Maafisa Watendaji wa Vijiji na Kata.
Akizungumza na www.gabrielkilamlya.blogspot.com Juu ya Suala Hilo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Bwana Valence Kabelege Amesema Kuwa Hatua Hiyo Imekuja baada ya Kubaini Kupungua Kwa Mapato Kutokana na Usimamizi Mdogo na Baadhi ya Watendaji Kuto Kuwa Waaminifu Katika Zoezi la
Ukusanyaji Mapato Hayo.Akizungumza na www.gabrielkilamlya.blogspot.com Juu ya Suala Hilo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Bwana Valence Kabelege Amesema Kuwa Hatua Hiyo Imekuja baada ya Kubaini Kupungua Kwa Mapato Kutokana na Usimamizi Mdogo na Baadhi ya Watendaji Kuto Kuwa Waaminifu Katika Zoezi la
Aidha Amesema Kuwa Majukumu Mengi ya Watendaji Yalikuwa Yakipelekea Baadhi ya Mapato Kutoroshwa na Hivyo Halmashauri Kukosa Mapato yake Ikizingatiwa Halmashauri Hiyo Kuwa na Kata 11 Pekee kati ya 28 Zilizokuwepo Hapo Awali.
Pamoja na Mambo Mengine Bwana Kabelege Amesema Kutokana na Mapato yatakayo patikana Kutoka Kwenye Kata Hizo Tatu Basi yatatoa Majibu ya Kubinafsisha na Kata Nyingine Zote au Kuendelea na Utaratibu wa Zamani Kuanzia Mwaka Mwingine wa Fedha.
Kwa Upande wake Afisa Uhusiano wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Bwana Lukelo Mshaura Amesema Endapo Suala Hilo na Makubaliano ya Mkataba na Mzubuni Huyo Yatakwenda Sawa Basi Itakuwa ni Karibu Mara Mbili ya Mapato yaliyokuwa Yakikusanywa na Maafisa Watendaji waliopo.