Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe ACP Fulgency Ngonyani Amethibitisha Kutokea Kwa Tukio Hilo.
Na Gabriel Kilamlya Njombe.
Mkazi Mmoja wa Ikang'asi Wilayani Njombe Isaka Kaberege Mwenye Umri wa Miaka 35 Amekutwa Amefariki Baada ya Kunywa Sumu ya Mahindi Aina Actelik Super.
Kamanda wa Polisi Mkoani Njombe ACP Fulgency Ngonyani Amesema Mwili wa Marehemu Umeoneka Ukiwa Kwenye Nyasi Ndefu Agosti 21 Mwaka Huu Majira ya Saa Nne Asubuhi na Kwamba Marehemu Hakuacha Ujumbe Wowote.
ACP Ngonyani Amesema Hadi Sasa Hakuna Mtu Yeyote Anayeshikiliwa Kuhusiana na Tukio Hilo na Kwamba Jeshi la Polisi Linaendelea na Uchunguzi Juu ya Tukio Hilo Huku Akitoa Wito Kwa Wananchi Kuacha Kujichukulia Maamuzi Yasiyofaa Ikiwemo Kujinyonga.