SHIRIKA LA KILIMO LA NADO NJOMBE KUFANYA TAMASHA LA JUKWAA LA WAKULIMA MAY 30 NA 31 IGWACHANYA.
Mkurugenzi wa shirika la maendeleo ya kilimo Mkoani Njombe NADDO Bwana John Wihallah akielezea Juu ya Tamasha la Jukwa la wakulima wilayani Wanging'ombe Mwezi huu.
Na Gabriel Kilamlya.
Nchini Shirika la Maendeleo ya Kilimo Mkoani Njombe NADDO linatarajia
kufanya maonesho ya Jukwaa la Wakulima Wilayani Wanging'ombe Ikiwa
ni Maandalizi ya Kuwapata Wakulima Bora Watakaoshiriki Maonesho ya
NaneNane Mwaka Huu Mkoani Mbeya
Akizungumza na Kituo hiki juu ya Jukwaa Hilo mkurugenzi wa Shirika la
NADDO Bwana John Wihallah amesema Takribani Wakulima Elfu Tano
waliopata Mafunzo ya Mashamba Darasa Mwaka Huu Watashiriki Katika
Jukwaa Hilo litakalofanyika Kwa siku mbili kuanzia mei 30 na 31 Mwaka
huu katika Ofisi za Shirika Hilo Zilizopo kwenye Makao makuu ya Wilaya
ya Wanging'ombe Kule Igwachanya.
Amesema kuwa jukwaa hilo litawapa Fursa wakulima katika Kutambua
changamoto zinazo wakabili ili kuangalia namna ya kuzipatia Ufumbuzi
kwa kushirikiana na Serikali.
Katika Hatua Nyingine Bwana Wihallah ameeleza kuwa kwa sasa tayari
wakulima wameanza kunufaika na mafunzo ya Mashamba Darasa
waliyokuwa wakiyapata pamoja na kujifunza Ujasiliamali ambao wamesha
anza kwa kutengeneza Sabuni,Batiki pamoja na ufugaji Kuku.
Hata hivyo katika kuwainua kiuchumi kutokana na Shughuli zao za Kilimo
amesema kuwa Shirika hilo tayari limefanikiwa kusajiri Taasisi ya Kifedha
ya SACCOS Itakayowasaidia kutumia katika ukopaji wa Fedha za miradi
mbalimbali.................................................................