WANAFUNZI WALIPUKIWA NA MABAKI YA BOMU NABOTI SEKONDARI MAKAMBAKO NJOMBE.
Baadhi ya Maeneo walimo jeruhiwa wanafunzi hao na Mmoja kupatwa na Mshtuko wa Mlipuko wa Mabaki ya Mabomu hayo kutokana na Tatizo lake la Moyo alilonalo na hivyo kupelekea wanafunzi Watano kulazwa Ilembula Hospitali.
Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi.Sarah Dumba akiwajulia Hali wanafunzi hao katika Hospitali ya Lutherani ya Ilembula.
Mwanafunzi Evance Joseph[16]kidato cha Kwanza ambaye alikuwa akifanya Majaribio ya Kuchoma Mabaki hayo ya Bomu huku Mengine akiyahifadhi kwenye Tranka lake la Nguo.
Wanafunzi wakiwa wanaendelea kufanyiwa Vipimo vya Mionzi ya Jua kutambua ukubwa wa Tatizo katika Hospitali ya Ilembula Wilayani Wanging'ombe Mkoani Njombe.
DC Njombe na Msafara Wake wakiwatazama Wanafunzi waliojeruhiwa na Mabaki ya Mabomu hayo.
Mwanafunzi aliyejeruhiwa Katika maeneo Mbalimbali ya Mwili wake ikiwemo Miguuni.
Hapa Mkuu wa Wilaya na Msafara wake ukiongozwa Na JWTZ Makambako.
Msafara ukiwasili katika Shule ya Sekondari NABOTI Iliyopo katika Halmashauri ya Mji wa Makambako.
Wanafunzi wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Njombe.
Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi.Sarah Dumba akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari NABOTI Mara baada ya kutoka katika Hospitali ya Ilembula kuwajulia Hali wanafunzi Watano waliolazwa kwa Matibabu.
Wanafunzi wa NABOTI Sekondari wakimsikiliza DC na Msafara wake.
Na Gabriel Kilamlya Njombe.
Wanafunzi Wanne wa shule ya sekondari NABOTI iliyopo katika Halmashauri ya Mji wa Makambako wamejeruhiwa na Mlipuko wa Mabaki ya Bomu huku mmoja akipata Mshtuko wa Moyo kutokana na Mlipuko huo Baada ya Wanafunzi Takribani saba wa Kidato cha Kwanza kwenda kuyaokota Mabaki hayo kwenye Mlima uliopo Jirani na maeneo ya Jeshi.
Tukio hilo limetokea may 23 majira ya Saa moja za Jioni baada ya wanafunzi wa Kidato Cha kwanza waliokwenda Kuokota
Mabaki hayo kuanza Kuyachoma.Tukio hilo limetokea may 23 majira ya Saa moja za Jioni baada ya wanafunzi wa Kidato Cha kwanza waliokwenda Kuokota
Mabaki ya Mabomu hayo yaliokotwa na Wanafunzi wa Kidato cha Kwanza waliokwenda kwenye Mlima uliopo Jirani na Shule hiyo na hivyo wakati wakiota Moto kwenye Bweni la Wavulana ndipo Wakaanza Kuyachoma moto wakitaka Kujaribu na kujua kama ni nini.
Aidha wanafunzi hao ni Pamoja na Evance Joseph mwenye umri wa Miaka 16 wa kidato Cha Kwanza ambaye ndiye aliyekuwa na Mabaki hayo huku Mengine Akieleza Kuyaacha kwenye Tranka Lake la Nguo Henry Chambilo[16]anayesoma kidato cha Pili,Cleofas Ngenyuko[15]Kidato Cha Pili,Allan Mbilinyi[14]Kidato cha Kwanza na Edgar Msanga[15]Mwanafunzi wa Kidato cha Tatu ambaye alipatwa na Mshtuko wa Moyo Baada ya Kulipuko kwa Mabaki ya Mabomu.
Akizungumza na www.gabrielkilamlya.blogspot.com akiwa Hospitali ya Ilembula Mwanafunzi huyo Evance Joseph ambaye alikuwa akifanya majaribio ya kuchoma Mabaki hayo bila Kujua amesema kuwa pamoja na kuyaokota mabaki hayo na mengine kuyahifadhi Bwenini kwenye Tranka lake lakini tayari baada ya mlipuko huo yameshatolewa hata aliyoyahifadhi.
Kufuatia Tukio hilo Mkuu wa Wilaya ya Njombe amelazimika kufika katika Hospitali ya Ilembula walikolazwa wanafunzi hao hadi Shuleni hapo kujionea hali halisi iliyopo hadi sasa na kuagiza Jeshi la Wananchi Makambako kufanya uchunguzi na kuyaondoa Mabaki Mengine yatakayo kuwepo katika Maeneo hayo.
Kwa Upande wake Meja Mbaga Kutoka Jeshi la Wananchi Makambako amewataka Wanafunzi hao kuwa Makini katika Maeneo yao na kwamba endapo watakuta kitu kigeni basi watoe Taarifa kwa Walimu wao.
Joseph Nyalusi ni Mkuu wa Shule ya Sekondari NABOTI ambaye amesema hadi sasa alisha wapiga Marufuku wanafunzi hao kufika Katika Maeneo hayo lakini Baadhi ya Wanafunzi wamekuwa wakikiuka agizo.
Hadi sasa Wanafunzi hao wamelazwa katika Hospitali ya Ilembula Wilaya ya Wanging'ombe Mkoani Njombe baada ya Kupigwa X-RAY ikiwa hali zao wote zinaendelea Vizuri.