Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

KAYA MASIKI KUUNDA VIKUNDI VYA UWEKAJI AKIBA NJOMBE

$
0
0
 Washiriki wa semina ya Siku tano ya mafunzo ya Uundaji Vikundi vya Uwekaji Akiba kwa kaya masikini TASAF III Kutoka Halmashauri ya Mji wa Njombe Wakiwa Kwenye Picha ya Pamoja na Viongozi wa TASAF Taifa Nje ya Ofisi za Halmashauri ya Mji wa Njombe

 Mwenyekiti wa Muda wa Semina Hiyo Mwalimu Stanley Kondola Ambaye ni Mratibu Elimu kata ya Lugenge Akizungumza Mara Baada ya Hotuba na Meneja Miundombinu TASAF

 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Iluminata Mwenda Akizungumza na Washiriki wa TASAF
 Meneja Miundombinu wa TASAF Makao Makuu Mhandisi Elisifa Kinasha Akisoma Taarifa ya Maendeleo ya TASAF III




Ephigenia Woisso ni afisa uratibu Tasaf Makao makuu ambaye amesema kupitia mpango huo kaya masikini ambazo zitafanikiwa kuunda vikundi hivyo zitanufaika sana


Baadhi ya Washiriki Kutoka Halmashauri za Ludewa na Njombe Mji Wakiwa Kwenye Semina

Na Gabriel Kilamlya NJOMBE

Serikali Nchini imeanzisha Mpango mpya wa kuunda vikundi katika kaya masikini kupitia mradi wa Tasaf awamu ya tatu kwa lengo la kuwasaidia walengwa kujenga uchumi endelevu kwa kujiwekea akiba.

Katika mkoa wa Njombe wajumbe toka maeneo mbalimbali wakiwemo wa ngazi ya kata wameanza semina ya siku tano ya namna ya kwenda kutoa elimu kwa wananchi wanaonufaika na mradi wa tasaf kupitia mpango wa  uhawilishaji fedha juu ya kwenda kuunda vikundi hivyo ambavyo vitawasaidia kujiwekea akiba ya fedha wanazopata.

Akizindua semina hiyo ya siku tano katika Halmashauri ya mji wa Njombe iliyojumuisha wajumbe toka halmashauri ya wilaya ya Ludewa na Njombe mji,Meneja miundombinu Tasaf makao makuu Mhandisi Elisifa Kinasha kwa niaba ya Mkurugenzi wa Tasaf Taifa Ladslaus Mwamanga amesema kupitia Tasaf awamu ya tatu zaidi ya kaya milioni moja zinalipwa fedha hadi sasa jambo lililoifanya serikali kuja na mpango wa kuweka akiba kupitia vikundi.


Ephigenia Woisso ni afisa uratibu Tasaf Makao makuu ambaye amesema kupitia mpango huo kaya masikini ambazo zitafanikiwa kuunda vikundi hivyo zitanufaika sana na
akiba watakazojiwekea kwani maeneo ambayo vikundi vimeshaundwa yameonesha mafanikio makubwa zaidi.



Kwa upande wake mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Njombe Iluminata Mwenda ambaye ni mwenyeji wa semina hiyo amewataka washiriki kutambua kuwa wao ndio watakaokwenda kuwa walimu wa kuwaelimisha wananchi na hivyo ni lazima kuzingatia kile watakachofundishwa.



Kwa asilimia kubwa mpango huo umekuja na sura ya kuwahusisha akina mama zaidi katika kuunda vikundi hivyo badala ya akina baba huku kwa kaya ambazo akinamama wataonekana kuwa wababe,Akina baba ndipo watakapohusishwa.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Trending Articles