Na Erasto Mgeni Ludewa
Mara baada ya mgombea wa ubunge jimbo la ludewa kupitia chadema Bathromeo msambichaka kushinda pingamizi aliyowekewa na mgombea ubunge kupitia chama cha mapinduzi Deo Filikunjombe mgombea huyo amezindua bkampeni za uchaguzi huku akiwahakikishia wananchi kushinda kwa kushindo
Msambichaka aliwekewa pingamizi na deo filikunjombe kwa madai ya kuwa alishindwa kurejesha fomu ya ubunge namba 10 sababu iliyomuondolea kigezo cha kuwa mgombea
Akiwa katika mkutano ulifanyika katika viwanja vya sokoni mjini Ludewa amesema katika mchakato wa ujazaji fomu yeye alikamilisha kila kilichohitajika na kuzirejesha fomu hizo na alishangazwa na kitendo cha tume kumtangaza deo Filikunjombe kuwa amepita bila kupingwa hali iliyomfanya kukosa imani na tume ya uchaguzi
Miongoni mwa vipaumbele vyake endapo wananchi watamchagua ni pamoja na swala la elimu,afya,miundombinu ya barabara na maji,uchumi wa mtu binafsi na pato la taifa
Hata hivyo msambichaka amewaomba wananchi kutoyumbishwa na wanasiasaa ambao wanatafuta madaraka na sio utumishi bali wathamini haki yao ya kidemokrasia kwa kumchagua kiongozi wanae mtaka huku akiwaomba wananchi kuonyesha ushirikiano
Kwa upande wake Emmanuel Kayombo akizungumza kwa niaba ya katibu wa chadema mkoa wa Njombe Bwana Alatanga nyagawa amesema chadema imejipanga kushinda kwa kishindo uchaguzi huo kuanzia ngazi ya udiwani mpaka ikulu
Kayombo amewaomba wananchi kuelekeza kura zao kwa wagombea wa ukawa kwani umoja huo umedhamilia kuleta mabadiliko nchini Tanzania
Kastory nziku ni mwenyekiti wa chadema wialaya ya ludewa ameseam chama hicho kimewasimamisha madiwani katika kata zote 26 lakini karibu kata zote ziliwekewa pingamizi akidai kuwa ni hujuma zilizofanywa na chama cha mapinduzi kwa kuwachomolea wagombea hao fomu namba kumi na kwamba mpaka sasa wamekwisha kuawndika barua ya kuomba mkurugenzi wa uchaguzi aondolewe katika wilaya hiyo ili kuondokaba na hujuma zinazoweza kujitokeza wakati wa uchaguzi
Hali imekuwa tofauti na ramani iliyochoreka katika akili za wananchi waliowengi zaidi kuwa hakuna mwamkoa mkubwa wa Chadema katika wilaya ya ludewa bali ukweli ni kwamba wananchi sasa wameamka na ktumia demokrasia yao kwa kujitokeza kwa wingi katika mkutano huo wa siasa kusikiliza sera ya mgombea wao