Maelfu ya Wakazi wa Mkoa wa Njombe Wakimsindikiza Edward Lowasa Kupumzika Mara Baada ya Kuhitimisha Mkutano Wake wa Kampeni Majira ya Saa 05:55 Jioni Katika Viwanja Vya Shule ya Mtakatifu Bakita Mjini Njombe Leo.
Na Gabriel Kilamlya Njombe
Mgombea Urais Kwa Tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Chini ya UKAWA Edward Lowasa Amezungumza na Wakazi wa Mkoa wa Njombe Katika Muendelezo Wake wa Kunadi Sera Zake Huku Akiwataka Wananchi Kuhakikisha Wanatumia Haki Yao ya Kikatiba Kumpigia Kura na Kulinda Kura Hizo Kwa Nguvu Zote.
Kauli Hiyo Ameitoa Akiwa Katika Viwanja Vya Shule ya Msingi Mtakatifu Bakita Ambapo Amesema Imekuwa ni Kawaida Kuibiwa Kwa Kura za Wananchi Mara Baada ya Kuzipiga na Kuwakosesha Haki Zao Jambo Ambalo Kila Mmoja Anapaswa Kukomaa Katika Kuzilinda.
Aidha Amesema Endapo Watanzania Watamchagua Kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Basi Atakwenda Kupambana na Changamoto Zinazowakumba Wananchi Likiwemo Tatizo Sugu la Wakulima Kukosa Haki Zao Wakiwemo Wakazi wa Lupembe Wanaolima Chai na Kuuza Kwa Hasara.
Katika Hatua Nyingine Aliyekuwa Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye Amesema Wao Wamelazimika Kukihama Chama Cha Mapinduzi CCM na Kuhamia UKAWA Baada ya Kuona Chama Cha Mapinduzi Hakiwezi Kuleta Mabadiliko ya Kweli Kwa Watanzania.
Sumaye Amesema Kitendo Cha Kuibiwa Wanyama Kama Twiga,Usafirishaji wa Dawa za Kulevya Ikiwa ni Pamoja na Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana Kueleza Kuwa Ndani ya Serikali Kuna Mawaziri Mizigo ni Ishara Kwamba Serikali Iliyopo Chini ya Chama Tawala Inahitaji Mabadiliko.
Hata Hivyo Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Laurence Masha Ambaye ni Mmoja wa Mawaziri Waliohama CCM na
Kuhamia Chadema Amewatahadharisha Wananchi na Wanahabari Nchini Juu ya Sheria ya Mtandao Ambayo Inaanza Kutumika Hapo Kesho Kuwa Kila Mmoja Anatakiwa Kuwa Makini na Anachokifanya Kupitia Mitandao Kwani Sheria Hiyo Imeandaliwa Kwa ajili ya Kulinda Maslahi ya Watu Wachache.