




………………………………………………………………………
Na Greyson Mwase, Nachigwea
Imeelezwa kuwa dawa ya migogoro katika umiliki wa leseni za madini Kanda ya Kusini, itapatikana baada ya ofisi ya madini iliyopo Nachingwea kuanza kutumia huduma za leseni za madini kwa njia ya mtandao.Hayo yalisemwa na Afisa Madini Mkazi kutoka Nachingwea Mayigi Makolobela alipokuwa akifungua mafunzo kuhusu huduma ya leseni za madini kwa njia ya mtandao yaliyoshirikisha wachimbaji wa madini katika wilaya za Ruangwa, Liwale na Nachingwea zilizopo mkoani Lindi.Makolobela alisema awali katika wilaya hizo kulikuwepo na migogoro ya umiliki wa leseni za madini iliyosababishwa na wamiliki wa leseni kuingiliana kwenye maeneo yao ya
kazi huku kila mmoja akidai ni mmiliki halali wa eneo husikaAlisema wakati mwingine, maombi ya leseni yalikuwa yanagongana kutokana na wamiliki tofauti kuomba eneo moja ambapo inapotokea aliyewahi kutuma maombi akapatiwa leseni, mwombaji anayefuatia hudai kuwa kuna upendeleo umefanyika.Alieleza kuwa katika mfumo huu mpya, mara baada ya maombi ya leseni kufanyiwa kazi kwa njia ya mtandao, mfumo hautaruhusu mwombaji mwingine kuomba leseni ya uchimbaji wa madini ya eneo husika.Alisisitiza kuwa mbali na kuondoa migogoro kwenye umiliki wa leseni za madini, mfumo huu utawezesha maombi mengi ya leseni za madini kufanyiwa kazi kwa haraka kwa kuwa maombi yote yatajazwa na waombaji wa leseni wenyewe.Wakati huohuo Makolobela alisisitiza waombaji wa leseni kufuata sheria na kanuni za madini wakati wa maombi na usimamizi wa leseni za utafutaji na uchimbaji wa madini.