Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Article 13

$
0
0
MKUU WA MKOA NJOMBE AWAAGIZA WATENDAJI WA HALMASHAURI KULIPATIA UFUMBUZI TATIZO LA KUZOROTA KWA UTALII.
 Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Njombe kulia ni DC Wanging'ombe Bi.Esterina Kilasi akifuatiwa na DC Ludewa Juma Madaha, Kulia Kwake ni DC Makete Bi.Josephine Matiro na Kushoto ni DC nJOMBE Bi.Sarah Dumba wakiwa kwenye Kikao cha Utalii leo.
 Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Njombe ikiwa kwenye Kikao cha Utalii leo Mjini Njombe.
 Baadhi ya Wadau wa Utalii mkoani Njombe wakiwa kwenye kikao cha Utalii katika Ukumbi wa Kyando Mjini Njombe Mwanzoni ni Afisa Utalii kanda ya Kusini Bwana
Gervas Mwashimaha.
 Hapa wadau wa Utalii Mkoani Njombe na kanda ya Kusini wakiwa kwenye Makundi kubainisha Vivutio vya Kuvipa Kipaumbele ndani ya Halmashauri.
 Afisa Nyuki wa Mkoa wa Njombe Bwana Daudi Kumburu mara baada ya kuwasilisha Maazimio ya vivutio vya Utalii Mkoani Njombe na Namna ya kukabiliana navyo.
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe Bi.Mgeni Baruani akibainisha Maazimio yaliyofikiwa katika utatuzi wa Vivutio na Changamoto zake jinsi ya kukabiliana nazo.
 Mratibu wa Mradi wa Utalii wa SPANEST Bwana Godwell olle Meng'ataki akiwashukuru wadau wa Utalii Mkoani Njombe na Kanda ya Kusini kiujumla kwa kukubali kujipanga kukabiliana na Changamoto za Kiutalii Nchini.
 Mkuu wa Mkoa wa Njombe Capt.Mstaafu Asseri Msangi akifunga Warsha ya siku Mbili ya Wadau wa Utalii Kanda ya Kusini mwa Tanzania.

Na Gabriel Kilamlya.

Mkoa wa Njombe umetoka na Maazimio mbalimbali ya kuweza kukuza na Kuboresha sekta ya Utalii Nchi pamoja na Kukuza Uchumi katika Taifa.

Miongoni mwa Maazimio hayo ni pamoja na kuangalia Vivutio vya kuvipa kipaumbele katika Wilaya zote Mkoani Njombe na Hivyo kuzifanyia Mchakato wa Kuviboresha katika Kukuza Uchumi na Pato la Taifa.

Akitangaza Maazimio hayo Wakati wa Kufunga Warsha ya Siku Mbili ya Sekta ya Utalii iliyokuwa Ikifanyika Mkoani Njombe Afisa Nyuki wa Mkoa wa Njombe bwana Daudi Kumburu amesema kuwa baadhi ya Vivutio hivyo ni pamoja na Maeneo ya Kihistoria ya Mdandu,Msitu wa Nyumbanitu na Kila Wilaya inatakiwa kutenga vivutio vyake na kuvifanyia Kazi.

Akifunga semina hiyo ya Siku Mbili iliyowakutanisha wadau wa Utalii kutoka Wilaya zote za Mkoa wa Njombe pamoja na wadau kutoka Kanda ya Nyanda za Juu kusini Mkuu wa mkoa wa Njombe ameagiza wakurugenzi na Wakuu wa Wilaya kuhakikisha wanafakisha kukuza vivutio vilivyobainishwa kila Wilaya huku Maafisa Utalii waliopo na watakao ajiriwa wabainishe mikakati hiyo na kuifikisha kwenye Mabaraza ya Madiwani.

Pamoja na Mambo mengine Captain Msangi amewataka watanzania Kujenga mazoea ya kuibua Vivutio tofauti na Mahotel yaliyozoeleka kama Kujenga ZOO za Wanyama Mkoani Njombe.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Trending Articles