SITTA AONYA VYOMBO VYA HABARI KUPOTOSHA UMMA JUU BUNGE LA KATIBA
Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba Samwel Sitta![]()
![]()
Mwenyekiti Wa Bunge Maalum La Katiba,Samuel Sitta Amevitaka Vyombo Vya Habari Nchini Kuacha Uchochezi Na Chuki Wakati Vinapohabarisha Umma Kuhusiana Na Mchakato Wa Katiba Mpya.
Kauli Hiyo Ameitoa Leo Wakati Alipokutana Na Baadhi Ya Waandishi Wa Habari Katika Viwanja Vya Bunge Mjini Dodoma Huku Akiviasa Vyombo Vya Habari Kuachana Kuandika Habari Zenye Kuleta Uchochezi Na Chuki Ili Kuvuruga Mchakato Wa Katiba Mpya.
Sitta Amesema Kuwa Kuna Baadhi Ya Watu Wamekuwa Na Dhana Tofauti Kuhusu Kazi Inayofanywa na Bunge Maalum La Katiba,Hivyo Ni Vema Kuepukana Nao Na Kuhabarisha Umma Taarifa Sahihi Ili Katiba Mpya Iweze Kupatikana.
Amesema Hadi Sasa Wajumbe wa Bunge Hilo Wanafanya Kazi Waliyotumwa Tena Kwa Uadilifu Mkubwa Hivyo Suala la Upotoshaji Halitakiwa Kupewa Nafasi Kwenye Vyombo Vya Habari
Aidha Sitta Ameongeza Kwa Kutolea Ufafanuzi Juu Ya Baadhi Ya Makundi Yaliyowasilisha Mapendekezo Yao Katika Bunge Hilo, Kwa Kusema Kuwa Maoni Yaliyopelekwa Na Makundi Mbalimbali Kwa Lengo La Kuboresha Rasimu Mpya Ya Katiba Yanapokelewa Lakini Sio Maoni Tu Ya Mtu Binafsi Au Mwananchi,Bali Wanapokea Maoni Kupitia Makundi Maalum Kama Yalivyo Kwa Wafugaji,Wasanii Na Wakulima Ambao Wameshawahi Kuwasilisha Maoni Na Mapendekezo Yao Kwa Iliyokuwa Tume Ya Mabadiliko Ya Katiba Lakini Hayakuonekana Na Mengine Yalisahaulika Katika Rasimu Hiyo.
Wakati Huohuo,Baadhi Ya Wenyeviti Wa Kamati Mbalimbali Za Bunge Hilo,Wamesema Tayari Wamemaliza Kazi Ya Kuchambua Rasimu Hiyo Vizuri Katika Kamati Zao.
Akizungumzia Kuhusu Kazi Hiyo,Mwenyekiti Wa Kamati Namba Tatu Ya Bunge Hilo, Dkt. Francis Michael Amesema Suala La Ardhi Lilionekana Kuwa Nyeti Katika Kamati Yake.
Dkt. Francis Ameongeza Kuwa Suala La Kupokea Mapendekezo Kutoka Kwa Makundi Mbalimbali Si Kwamba Kila Kitu Kitawekwa Kwenye Katiba Mpya Bali Ni Yale Mambo Ya Msingi Pekee.
Naye Mwenyekiti Wa Kamati Namba Moja Ya Bunge Hilo, Ummy Mwalimu Ally Na Makamu Mwenyekiti Wa Kamati Namba Kumi Na Moja, Hamad Massauni Wamesema Kuwa Katika Kamati Zao Majadiliano Yalikwenda Vizuri.
……………………………………………………………………………………………………