Sudan yaunda mahakama juu ya jinai za Darfur
Mkuu wa vyombo vya mahakama wa Sudan ametoa amri ya kuundwa mahakama maalum kwa ajili ya kushughulikia jinai hatari zilizofanywa katika eneo la Darfur magharibi mwa nchi hiyo. Mahakama hiyo itasimamiwa na al Aman al Twibi al Bashir Jaji wa Mahakama Kuu ya Sudan na majaji wengine wawili wataunda mahakama ya rufaa. Â
Mpango wa kuunda mahakama maalum ya kushughulikia jinai za Darfur kwa lengo la kutekeleza uadilifu unatekelezwa ikiwa ni baada ya kupita miaka minne tangu Rais Omar al Bashir Sudan alipoafiki kuasisiwa mahakama 3 za jinai katika miji ya Fashar, Niyala na al Janiyah kwenye jimbo la Darfur.
Katika upande mwingine maafisa wa Sudan na Ethiopia wamekubali kupeleka kikosi cha pamoja katika mpaka wa nchi mbili hizo.Â
Kamati ya pamoja ya ulinzi ya Sudan na Ethiopia imekubaliana juu ya kuundwa kikosi cha pamoja na kupelekwa katika maeneo 8 ya mpaka wa nchi mbili hizo ili kuimarisha amani na usalama na pia kupeleka mbele maendeleo ya pande mbili.