Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Article 8

$
0
0

WATU WAWILI MBARONI KWA TUHUMA ZA KULIPUA BOMU NA KUJERUHI NANE JIJINI ARUSHA

 mmoja wa mtu alielipuliwa na bomu katika mgahawa wa
Traditional Indian Cusine aliyejukilana kwa jina la Deepak Gupta (25)
akiwa amelazwa  katika hospitali ya seliani ndani ya  chumba cha
mahututi (ICU) mara baada ya kukatwa mguu wake mmoja wa kushoto
kutokana na mguu huo kuumizwa sana na bomu hilo.

 Mtoto   Manci  Gupta akiwa amelala anasikilizia maumivu ya miguu  aliyoumia mara baada ya kulipukiwa na bomu yeye na familia yao wakati wameenda kupata chakula cha usiku katika mgahawa huo
 mama Munisha Gupta (42) pamoja na mme wake Mahush
Gupta (42) akiwa wameegemeana wote wamezurika katika mlipuko wa bomu hilo wakati wameenda kupata chakula cha usiku
 picha ikionyesha askari wa jeshi la wananchi  kitengo cha mabom wakiwa
katika eneo la tukio ambalo bumu lilirushwa  ndani ya mgahawa wa
ujulikanao kwa jina la Traditional Indian Cusine  ulipo pembeni ya
hotel ya gmkana.
 muonekano wa eneo la tukio.

 SEHEMU ambayo inasemekana bomu  lilitua mara baada ya kutupwa.

Mkurugenzi wa tiba ambaye pia ni kaimu mgamga mkuu wa hospitali ya Seliani Dr. Paulo akiongea na waandishi wa habari.Jeshi la Polisi Nchini Linawashikilia Watu Wawili Kwa Tuhuma za Kuhusika na Shambulio la Bomu Kwenye  Mgahawa wa WAMA BAMA Uliopo Katika Eneo la Jimkana Jijini Arusha.

Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai DCI Issaya Mburu Amesema Kuwa Watuhumiwa Hao Wamekatwa Jijini Arusha Kwa Tuhuma za Kuhusika na Tukio Hilo Lililojeruhi Watu Nane.

Aidha Amesema Jeshi Hilo Linawashikiliwa Watuhumiwa  Wengine Sita Kwa Tuhuma za Kuhusika na Mlipuko Uliotokea Wiki Iliyopita na Kumjeruhi Kiongozi wa Dini Sudy Ally Sudy.

DCI Nguru Amesema Kuwa Kwa sasa Jeshi Hilo Linaendelea na Msako wa Nchi Nzima Kuwatafuta Zaidi ya Watuhumiwa 25 wa Matukio ya Milipuko ya Mabomu Katika Maeneo Mbalimbali Ikiwemo Jiji la Arusha, na hapa anaeleza.

Cue.....Mburu

Aidha Amewataka Wananchi Kuwa Makini na Mikusanyiko ya Watu na Kwamba Waandaaji wa Mikusanyiko Hiyo Kuchukua Tahadhari za Kiusalama.
        

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Trending Articles