Mbunge Filikunjembe na Mafulu wakipongezwa kwa kuteuliwa walezi wa UWT Njombe
Dr Suzana Kolimba wa tatu kushoto akipongezwa kwa mchango wake UWT |
walezi wa UWT mkoa wa NJombe mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe ( kulia ) na mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Lediana Mafulu wakipongezana kwa kuteuliwa kuwa walezi wa UWT mkoa wa Njombe |
Mbali ya Filikunjombe kuendesha harambee hiyo kwa yeye mwenyewe kuchangia milioni 10 kwa ajili ya kuchangia ununuzi wa gari hilo pia mjumbe wa bunge la katiba ambae ni mchumi wa UWT mkoa wa Njombe Dr Suzana Kolimba alichangia kiasi cha Tsh milioni 5 katika harambee hiyo.
Akizungumza baada ya kuendesha harambee hiyo na kusimikwa kuwa mlezi wa UWT mkoa wa Njombe pamoja na mbunge Lediana Mafulu Mng’ong’o mbunge Filikunjombe alisema kuwa lengo la kuchangisha fedha hizo ni kuiwezesha UWT Njombe kuwa na
gari lake la kisasa ambalo litasaidia kuendesha shughuli za jumuiya hiyo.
gari lake la kisasa ambalo litasaidia kuendesha shughuli za jumuiya hiyo.
“Nilipopokea taarifa za kuteuliwa na Jumuiya yenu kuwa Mlezi, kwanza nilishituka, msituko nilioupata haukuwa wa kuogopa majukumu bali ulikuwa ni mshituko wa tafakuli niliyoifanya juu ya uzito na hadhi ya nafasi hii ya Ulezi, maana sisi sote tunaonekana katika sura ya Uongozi wa Taifa na dunia tumezaliwa na wanawake na asilimia kama 99% tumelelewa na wanawake. Kwa hiyo swali gumu nililokuwa najiuliza ni
namna gani ninaweza kuwalea watu wenye uzoefu mkubwa wa kulea watu kuanzia mimba, kuja mtoto hadi kufikia hatua akaweza kuwa rais au Waziri. Uzoefu huo wanao akina mama tena chini ya uangalizi na uvumilivu mkubwa. “
Filikunjombe alisema kuwa anatambua vema nafasi na wajibu wa akina mama katika ujenzi wa CCM Imara, kama vile historia ya nchi yetu tokea Uhuru ilivyoainisha mchango mkubwa wa akina mama wakati wa kutafuta Uhuru wa nchi yetu, michango kama ya akina Bibi Titi Mohamed wakati wa harakati za Chama cha TANU kutafuta Uhuru wa Tanganyika.
“Zaidi ya hilo taarifa za kiutafiti zinaonyesha kuwa kura nyingi za ushindi za CCM tokea tulipoingia kwenye mfumo wa Vyama vingi mwaka 1992 ni za Wanawake, maana wanawake wanamsimamo, hawayumbi na wanajua wao ni Waathirika wa kwanza nchi inapoingia kwenye machafuko. “
Hata hivyo alisema kuwa moja kati ya mkakati wake kama mlezi wa UWT mkoa wa Njombe ni kuona mkoa hao unakuwa mkoa wa pekee kwa kutoruhusu upinzani kuchukua nafasi
“ Kazi yangu kama mlezi ni kuhakikisha naitumikia vema nafasi hii na kuhakikisha kupitia jumuiya hii mbengu mbovu ya upinzani ambayo imejipachika katika mkoa wetu inaondoka haraka iwezekanavyo na mwaka 2015 mkoa wa Njombe wote unakuwa na wa CCM.
Huku mchumi wa wilaya hiyo Dr Suzana Kolimba mbali ya kuchangia kiasi hicho cha Tsh milioni 5 kwa ajili ya kuunga mkono jitihada za mlezi Filikunjombe pia alisema kuwa lengo lake kama mchumi ni kuona mkoa huo wa Njombe hasa wanawake wanaendelea kuwa na uchumi imara .
Kwa upande wake mlezi Mafulu pamoja na kuipongeza jumuiya hiyo ya UWT kwa kumteua Filikunjombe nay eye kuwa mlezi alisema kuwa bado jumuiya hiyo haikukosea kuwateua kwani wao ni miongoni mwa watendaji wazuri katika chama hicho.
Mbunge wa Mwibala Kangi Lugola