Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276
↧

Article 4

$
0
0
 Taswira ya Mji wa Njombe na Mazingira Yake.
Kaimu Meneja Mkuu wa Chama Kikuu Cha Ushirika Mkoa wa Njombe[NJORECU]Bwana Thomas Nyamba Akisoma taarifa ya Bodi ya Ushirika Huo.

Na Gabriel  Kilamlya Njombe

Chama Kikuu cha Ushirika Mkoani Njombe NJORECU Kimeelezea Mafanikio Yake Katika Kipindi cha Mwaka 2013 Ikiwemo Kuhamasisha  Wakulima Kuboresha Kilimo Ili Mazao Wanayozalisha Yaweze Kupata Soko la Uhakika.

Aidha Chama Hicho Pia Kimefanikiwa Kutembelea na Kukagua Mali Zinazomikiwa na NJORECU Yakiwemo Maghala , Majengo Yanatumiwa na Wapangaji Katika Wilaya za Mkoa wa Njombe Pamoja na Ghala Lililoko Mkoani Iringa.

Akizungumza na mtandao huu Pembeni Mara Baada ya Kumalizika Kwa Mkutano Mkuu wa NJORECU 

Kaimu Meneja Mkuu wa Ushirika Huo  Thomas Nyamba Amesema KwasasaUshirika Huo Umeonekana Kuwa na Uhitaji Mkubwa wa Wakulima na Kwamba Viongozi wa NJORECU

Wanatakiwa Kuwatembelea Wakulima Hao

Katika Maeneo Yao na Kutoa Elimu.

Bwana Nyamba Amesema Pamoja na Mafanikio Hayo Lakini Chama Hicho Kinakabiliwa na  Changamoto

Kadhaa Ambazo Baadhi Zimeanza Kutatuliwa Kwa Kununua Vitendea Kazi Ili Kuepusha Usumbufu na

Gharama Zisizo za Lazima Ikiwemo Kompyuta na Printa Kwa Ajili ya Kutunza Kumbukumbu za Ofisi.

Katika Hatua Nyingine Kaimu Meneja Huyo Mkuu wa NJORECU Amesema Hivi Sasa Chama Hicho

Kinaendelea na Ukarabati wa Ofisi Zakena Kwamba Zinatarajia Kukamilika Agosti Mwaka Huu na Kwamba

Chama Hicho Kimefanya Uhakiki wa Mali za NJOREKU Katika Maeneo Yote.

Pamoja na Mambo Mengine Lakini Pia Chama Hicho Kimefanikia Kununua Baadhi ya Vitendea Kazi Ili

Kuepusha Usumbufu na Gharama Zisizo za Lazima Ikiwemo Kompyuta na Printa Kwa ajili ya Kutunza

Kumbukumbu za Ofisi.

Pamoja na Mambo Mengine Chama Hicho Kikuu cha Ushirika Kimefanikiwa Kutembelea Maeneo Yote Ziliko

Mali Za Ushirika Huo Likiwemo Ghala Lililopo Mkoani Iringa Pamoja na Maeneo Mbalimbali Katika Wilaya za Mkoa wa Njombe.
↧

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Latest Images

Trending Articles