Deo sanga Awa Mgeni Rasmi.

Mbunge Deo Sanga Ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Njombe
Na Gabriel kilamlya Wanging'ombe
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Njombe Bwana Deo Sanga Ameweka Jiwe la Msingi Kwenye Ujenzi wa Madarasa Katika Shule ya Msingi Mambegu Wilayani Wanging'ombe Huku Zaidi ya Shilingi Milioni Kumi Zikipatikana Katika Harambee Iliyoendeshwa Kwa Ajili ya
Kuchangia Ujenzi Shule Hiyo
Akiongea Mara Baada ya Kuweka Jiwe la Msingi Katika Shule Hiyo Kwa niaba ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Njombe, Katibu wa Chama Hicho Mkoani Njombe Hosea Mpagike Amesema Fedha Hizo Zitatumika Katika Ujenzi na Ukarabati wa Madarasa Katika Shule ya Msingi Mambegu .
Aidha Mpagike Amewataka Wananchi Kushirikiana na Serikali Katika Shughuli Mablimbali za Maendeleo Ikiwemo Kuchangia Michango Miradi Inayotekelezawa na Kuanzishwa Katika Maeneo Yao.
Akielezea Hali ya Shule Hiyo Mratibu Elimu Kata wa Luduga Gibson Sauga Amesema Inakabiliwa na Chanagamoto Mbalimbali Ikiwemo Uhaba wa Walimu, Nyumba za Walimu Pamoja na Uchakavu wa Majengo.
Mbunge Deo Sanga Wa Jimbo la Njombe Kaskazini Achangia Shilingi Laki Nane na Mbunge Gerson Lwenge Kutoka Jimbo la Njombe Magharibi Akichangia Shilingi Laki Tano
...........................................................................................................................................