Baadhi ya Pikipiki zilizotolewa na mbunge wa Makambako Deo Sanga[JAH PEOPLE]Kwa wakazi wa Jimbo la Lupembe ambalo awali lilikuwa Jimbo Lake Kabla ya Kugawanywa.

Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi ccm ngazi ya kata na matawi Katika Jimbo la Lupembe Waliokusanyika kupokea Msaada wa Pikipiki na Baiskeli
Mbunge wa Jimbo la Makambako Deo Sanga[JAH PEOPLE] Akizungumza na wakazi wa Jimbo la Lupembe alipokwenda kugawa baiskeli na Pikipiki walizoomba viongozi wa CCM Ngazi ya Kata na Matawi.
Mbunge wa jimbo la Lupembe Joram Hongori akizungumza na wakazi wa kijiji cha Matembwe
Na Gabriel Kilamlya Njombe
Jumla ya Shilingi Milioni 74 Zimetumika Kununulia Pikipiki 23 na Baiskeli 217 Ambazo Wamegawiwa Viongozi wa CCM Ngazi ya Kata na Matawi Katika Kata za Tarafa za Mtwango na Lupembe Zilizotolewa na Mbunge wa Zamani wa Jimbo la Lupembe Deo Sanga Ambaye Kwa Sasa ni Mbunge wa Jimbo la Makambako.
Nyenzo Hizo za Usafiri Zimetolewa na Mbunge Sanga Katika Maeneo ya Matembwe na Kichiwa Ambapo Ameongozana na Mbunge wa Jimbo la Lupembe Joram Hongori Vitendea Kazi
Ambavyo Viongozi Hao Waliviiomba Ili Viwasaidie Kurahisisha Kazi ya Kukijenga Chama Hicho.
Awali Akizugumza Wakati wa Zoezi la Kugawa Pikipiki na Baiskeli Hizo Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Njombe Sadakati Kimati Amesema Kuwa Licha ya Kutolewa Kwa Vitendea Kazi Hivyo Lakini ni Moja ya Zoezi la Uimarishaji Chama Kwa ajili ya Kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020.
Mbunge wa Jimbo la Lupembe Joram Hongori Amesema Anaamini Msaada Huo Uliotolewa na Mbunge Wao wa Zamani Utasaidia Kuimarisha Chama na Kusimamia Vyema Katika Utekelezaji wa Ilani ya Chama Tawala Kwa Ushirikiano Baina Yake na Wao.
Akizungumza Mara Baada ya Kugawa Vitendea Kazi Hivyo Mbunge Deo Sanga Toka Jimbo la Makambako Ambaye Pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Njombe Amesema Anatarajia Pikipiki Hizo Zitasaidia Kuwafikia Wanachama Katika Maeneo Yote na Kwamba Hatarajii Zilete Mitafaruku Ndani ya Chama Hicho.
Kwa Upande Wao Baadhi ya Mkatibu Kata wa Chama Hicho Waliozungumza na Kituo Hiki Mara Baada ya Kupokea Pikipiki Hizo Wamesema Wanamshukuru Mbunge Sanga Kwa Kuwapa Msaada Huo Kwani Awali Walikuwa Wakishindwa Kuyafikia Maeneo Yote Kwa Wakati Kutokana na Changamoto za Kiusafiri na Kwamba Kwa Sasa Watafanya Kazi Hiyo Kwa Urahisi Zaidi.